Aliyemzuilia msichana miaka 2 Japan akamatwa

Kompyuta Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi wakibeba kompyuta ya Kabu Terauchi

Polisi nchini Japan wanamzuilia mwanamume wa umri wa miaka 23 anayetuhumiwa kumzuilia mateka msichana kwa miaka miwili jijini Tokyo.

Msichana huyo wa umri wa miaka 15 alifanikiwa kutoroka na kuwafahamisha polisi baada ya mwanamume huyo kutoka na kusahau kufunga mlango.

Polisi walimkamata mwanamume huyo kilomita 100 kutoka mji wa Tokyo katika jimbo la Shizuoka.

Inaaminika alijaribu kujiua.

Haki miliki ya picha AP

Mwanamume huyo anadaiwa kumteka nyara msichana huyo Machi 2014 akijifanya kuwa wakili aliyekuwa akishughulikia kesi ya talaka ya wazazi wake.

Polisi walitoa kibali cha kukamatwa kwa mwanamume huyo aliyetambuliwa kama Kabu Terauchi Jumapili.

Msichana huyo hajaonekana kudhuriwa kwa njia yoyote, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.