Meneja wa kampeni ya Donald Trump ashtakiwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Donald Trump

Meneja wa kampeni ya mgombea wa urais nchini Marekani kupitia tiketi ya chama cha Republican Donald Trump , ameshtakiwa kwa kumshambulia mwandishi wa habari katika mkutano wa kampeni.

Bwana Corey Lewandowski ameshtakiwa kwa shambulio dhidi ya aliyekuwa mwandishi wa Breitbart Michelle Fields.

Mnamo tarehe 8 mwezi Machi Bwana Lewandowski alimvuta na kumuangusha chini alipojaribu kuuliza swali na kujeruhiwa mkono.

Bwana Lewandowski anapanga kukana shtaka hilo,ilisema timu ya kampeni za bwana Trump