EgyptAir: Mtekaji ataka kumuona ''mkewe''

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndege ya EgyptAir

Ripoti zinasema kuwa mtekaji wa ndege ya EgyptAir anataka kuongea na mkewe walietengana naye anayeishi Cyprus ambaye kwa sasa anadaiwa kuelekea katika uwanja huo wa ndege.

Rais wa Cyprus Nicos Anastasiades amewaambia waandishi wa habari kwamba tukio hilo la utekaji nyara halikuwa la kigaidi,''tunafanya juhudi kuhakikisha kuwa kila mtu anawachiliwa akiwa salama'',aliongezea.

Akijibu maswali ya waandishi iwapo mtekaji huyo alishinikizwa na mapenzi,alicheka na kusema,''kila mara kuna mwanamke anayehusishwa''.

Shirika la habari la Cyprus CYBC linasema kuwa mtekaji huyo huenda alikuwa na malengo yake ya kibinafsi ,mtekaji huyo alikuwa na mkewe waliyetengana nchini Cyprus ,lilisema CYBC.

Walioshuhudia wanasema kuwa mtekaji huyo alirusha barua katika uwanja huo wa ndege ilioandikwa kiarabu akiomba ipelekwe kwa mwanamke huyo.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Ndege ya EgyptAir

Mtaalam wa maswala ya angani David Learmont ameiambia BBC kwmba rubani huyo angekataa kufuata amri ya mtekaji huyo.

''Tunaona kitu kisicho cha kawaida hapa.Rubani aliyetii amri ya mtekaji huyo kwa kuambiwa kwamba kulikuwa na mtu aliyvaa vilipuzi angekuwa na ushahidi wa kutosha kujua kwamba haingewezekana na kwamba hasingefuata amri ya mtekaji huyo."