Ulaya kuinyima jeshi la Burundi fedha

Image caption Ulaya kuinyima jeshi la Burundi fedha

Mabalozi wa umoja wa ulaya wamenukuliwa akisema kuwa umoja huo unapanga kupunguza ufadhili wa kikosi cha kijeshi cha Burundi kilichoko Somalia kama njia ya kumpa shinikizo rais Pierre Nkurunziza.

Mabalozi hao wa umoja wa ulaya wanasema kuwa hawatatuma pesa hizo kwa serikali ya Burundi tena kama ilivyokuwa ikifanyika hapo nyuma.

Jamii ya kimataifa inamshinikiza rais Nkurunziza kufanya mazungumzo na vyama vya upinzani vilivyopinga kuwania kwake kwa muhula wa tatu ilikuepuka vita ambayo vinatokota.

Malipo ya asilimia 20% ya fedha zinazolipwa kwa taifa linalochangia wanajeshi imekatwa wanasema.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Malipo ya asilimia 20% ya fedha zinazolipwa kwa taifa linalochangia wanajeshi imekatwa wanasema.

Aidha takwimu zinaonesha kuwa Burundi hupokea takriban dola miliono 13 kila mwaka kutoka kwa muungano wa ulaya kwa kuchangia wanajeshi wake kwa kikosi cha Amisom.

Takriban wanajeshi 5,000 wa Burundi wanashiriki katika operesheni hiyo ya kuilinda serikali ya Somalia isishambuliwe na wanamgambo wa Al shabab.

Wanajeshi hao wa Burundi ni miongoni mwa wanajeshi 22,000 wa AMISOM walioko somalia.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kumekuwa na machafuko tangu maandamano yalipotibuka mjini Bujumbura kupinga kauli ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Mataifa mengine yaliyochangia wanajeshi katika kikosi hicho ni pamoja na Kenya na Uganda.

Kumekuwa na machafuko tangu maandamano yalipotibuka mjini Bujumbura kupinga kauli ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Umoja wa mataifa unakisia kuwa takriban watu 4,00 wameuawa katika makabiliano kati ya wafuasi wa upinzani na vyombo vya usalama.