Mtoto wa kwanza katika mji, Italia tangu 1987

Haki miliki ya picha iStock
Image caption Mtoto wa kwanza katika mji, Italia tangu 1980

Wenyeji wa mji mmoja mdogo nchini Italia wamekuwa wakisheherekea kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza mjini humo tangu miaka ya 1980.

Meya wa mji wa Ostana, ulioko Kaskazini mwa Italia ambayo iko katika maeneo ya milima ya Piedmont aliwaongoza wenyeji kusherehekea ndoto yao kukamilika kwa kuzaliwa kwa kizazi kipya.

Ostana imeshudia kupungua kwa idadi ya wenyeji wake katika karne iliyopita kwa hivyo kuzaliwa kwa ''Pablo'' katika hospitalini moja ya Turin imeongezea idadi ya wenyeji kufikia 85.

Image caption Mji wa Ostana unajumla ya wenyeji 85 pekee

Jarida la La Stampa linasema japo wanasheherekea sio wote wanaoishi mjini humo.

Meya Giacomo Lombardo anasema kuwa miaka ya nyuma Ostana ilikuwa na wenyeji 1,000 lakini idadi hiyo ya watu imekuwa ikipungua kila kukicha hadi kufikia 85 sasa.

''Mara ya mwisho mtoto kuzaliwa hapa ni mwisho wa mwaka wa 1987''

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wazazi wa Pablo, Silvia na Jose walikuwa wamepanga kuondoka Italia kabla ya wenyeji kuwapa nafasi ya kuwa meneja wa uhifadhi wa misitu Ostana.

''Kati ya mwaka wa 1975 -1976 watoto 17 walizaliwa hapa''

Kwa sasa wenyeji wa mji huo wa Ostana wameanza kuweka mikakati ya kuimarisha idadi ya watoto wanaozaliwa kwa kuunda nafasi mpya za kazi.

Wazazi wa Pablo, Silvia na Jose walikuwa wamepanga kuondoka Italia kabla ya wenyeji kuwapa nafasi ya kuwa meneja wa uhifadhi wa misitu Ostana.

Kwa sasa wanapiga msasa sheria itakayowaruhusu wenyeji wasilipe kodi mbali na kutoa nyumba za bure kwa wenyeji wanaotafuta kazi.