Ajali ya ndege yawaua watu 7 Canada

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ndege ilioanguka nchini Canada

Watu saba wamefariki baada ya ndege moja ya kibinafsi kuanguka katika kisiwa cha mashariki ya pwani ya Quebec.

Mamlaka imesema kuwa ndege hiyo ilianguka ilipokuwa ikikaribia uwanja wa ndege wa Madeleine huku kukiwa na upepo mkali pamoja na barafu.

Jean Lapierre,aliyekuwa waziri wa uchukuzi nchini Canada pamoja na watu wa familia yake walikuwa miongoni mwa waathiriwa.

Bwana Lapierre mwenye umri wa miaka 59,alifanya kazi kama mchanganuzi wa CTV pamoja na vyombo vyengine vya habari.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Ndege ilioanguka Quebec Canada

Mojawapo ya vituo hivyo TVA kilisema mkewe Lapierre ,nduguze wawili na dadaake mmoja walifariki katika ajali hiyo.