India yakana kuipeleleza Pakistan

Image caption Mtu anayedaiwa kuwa mpelelezi wa India

Serikali ya India imekana madai ya Pakistan kwamba imemkamata mpelelezi wa India katika mkoa wa Balochistan.

Mamlaka ya Pakistan siku ya Jumanne ilitoa ukanda wa video ambao unaomuonyesha mtu mmoja akikiri kwamba alihusika na vitendo vya upelelezi.

''Hakuna ushahidi wa wazi kwamba India imekuwa ikiingilia maswala ya Pakistan'', msemaji wa jeshi Luteni Jenerali Asim Bajwa alisema.

Delhi imesema kuwa mtu huyo ni raia wa India,lakini ikakana madai ya upelelezi ikisema ''alifunzwa''.

Serikali ya India imekana madai kwamba mtu huyo alihusika na vitendo vya upelelezi nchini Pakistan kwa niaba yake,msemaji wa maswala ya kigeni Vikas Swarup alisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Bwana Swarup aliongezea kwamba India ina wasiwasi kuhusu afya ya mtu huyo na kuongezea kwamba licha ya ombi lake kutaka kuzungumza na raia huyo aliyekamatwa katika taifa la kigeni kama inavyotakikana kimataifa,Pakistan haijafanya hivyo.