UN yakataa ombi la DRC kupunguza Monusco

Haki miliki ya picha AFP
Image caption UN yakataa ombi la DRC kupunguza Monusco

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limepinga ombi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ipunguze idadi ya majeshi wa kulinda usalama MONUSCO walioko DRC.

Waziri wa mambo ya nje ya DRC alikuwa ameiambia baraza hilo la UN kuwa taifa hilo lingependa idadi ya majeshi wa Monusco; 20,000 ipungue kwa asilimia 50%.

Hata hivyo baraza hilo lilipinga ombi hilo na badala yake likaidhinisha ripoti iliyowasilishwa na mwanachama wake Ufaransa, iliyotaka idadi hiyo 20,000 iendelee kuwepo huko kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi vile ilivyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Baraza la uslama la umoja wa mataifa linataka idadi ya majeshi wa Monusco 20,000 iendelee kuhudumu DRC

Balozi wa Ufaransa katika umoja wa mataifa, Francois Delattre, alisema kuwa DR Congo "ingali inakabiliwa na changamoto tele na hivyo ni wajibu wa jamii ya kimataifa kuisaidia nchi hiyo kukabiliana nayo''

DR Congo imeratibiwa kufanya uchaguzi wake mkuu mwezi Novemba.

Katiba ya nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati inamruhusu rais wa sasa Joseph Kabila kuwania muhula mwengine.