Sunderland kusitisha mkataba wa Eboue

Image caption Emmanuel Eboue

Klabu ya Sunderland inatarajiwa kusitisha mkataba wa mlinzi wake Emmanuel Eboue, baada ya kupigwa marufuku na shirikisho la kandanda duniani FIFA kutoka kwa shughuli zozote zinazohusu kandanda kwa muda wa mwaka mmoja.

Eboue raia wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 32, alipigwa marufuku baada ya kushinda kulipa pesa alizokuwa akidaiwa na ajenti wake wa zamani.

Sunderland ilisema kuwa Eboue hakukijulisha klabu kuhusu suala hilo linalotajwa kuwepo tangu mwezi Julai mwaka 2013.