Risasi zalia Libya alipowasili Waziri Mkuu

Haki miliki ya picha
Image caption Waziri Mkuu wa Libya Fayez al Sirraj

Kumekuwa na milio ya risasi katika maeneo mbali mbali ya mji wa mkuu wa Libya Tripoli kufuatia kuwasili kwa njia ya bahari Waziri Mkuu Fayez Seraj pamoja na mafaasa wengine wa serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa.

Wakati wakiwasili walikumbana na upinzani mkali kutoka kundi lililojitangazia madaraka linalodhibiti mji huo wakidai kuja kwao ni jaribio la mapinduzi.

Kituo cha televisheni cha libya Al Naab kimefungwa na kimezuiwa kutangaza ambapo pia makao makuu yake yameshambuliwa na watu wenye silaha.

Mamlaka iliyojitangazia utawala katika mji mkuu wa Tripoli wamekuwa wakisema mipango inayofanywa na baraza la rais ni jaribio la mapinduzi ambapo baadhi wamesema watu hao wakamatwe.

Katika mkutano na waandishi wa habari katika ngome ya kikosi cha majeshi ya majini Waziri Mkuu Fayez Seraj amesema huu ni mwanzo wa ukurasa mpya.

"Tunamshukuru Mungu tumefika salama hapa Tripoli pamoja na changamoto tulizokutana nazo. Mpango wetu ni kuunganisha walibya pamoja na kuwepo kwa mpasuko. Vijana wetu ndio watakaoijenga Libya na kuipigania. Mungu atubariki sote." Alisema.

Nayo Wazara ya Mambo ya nje ya Marekani imetoa wito kwa pande zote nchini Libya kufanya kazi pamoja na kutafuta suluhisho ya mvutano wa kisasia. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje John Kirby amesema pande zote zinapaswa kufanya na kutafuta mstakabali wa amani ya Libya.