UN yachunguza dhuluma za kimapenzi CAR

Image caption Walinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Maafisa wa umoja wa mataifa wanachunguza madai ya kustaajabisha kuhusu unyanyasaji ya kingono uliofanywa na walinda amani nchini Jamhurui ya Afrika ya kati.

Mwaka uliopita kuliibuka madai 69 ya ubakaji wa watoto na dhuluma zingine za kimapenzi zilizofanywa na walinda amani kutoka mashirika kumi.

Shirika moja linasema kuwa limewasilisha ripoti mpya kwa umoja wa mataifa kuwa mwanajeshi mmoja aliwalazimisha wasichana wanne kufanya mapenzi na mbwa.