Boko Haram laapa kutosalimu amri

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Abubakar Shekau

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram wametoa kanda mpya ya video wakiapa kuendeleza vita vya kutaka uongozi wa sheria za kiislamu.

''Lazima mujue kwamba hakuna ukweli ,hakuna majadiliano,hakuna kusalimu amri'', alisema mtu mmoja aliyejifunika uso na kuzungumza kwa lugha ya hausa.

Ujumbe huo unajiri baada ya kanda ya video isiojulikana mwezi uliopita kumuonyesha kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau akionekana dhaifu swala linaloongeza uvumi kwamba mda wake katika uongozi wa kundi hilo unaelekea ukingoni.

Katika kanda hiyo ya video kuna watu wamesimama na bunduki za AK-47 mbele ya magari .