Mtoto wa miaka 8 akwama uwanja wa ndege

Image caption Alikamatwa wakati alisafiri peke yake kutoka chini Comoro akitumia pasipoti ambayo haikuwa yake

Mtoto mmoja wa kiume amekwama kwenye uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle mjini Paris nchini Ufaransa, tangu tarehe 21 mwezi machi baada ya kushindwa kuingia nchini ufaransa wala kurudi nyumbani.

Mtoto huyo wa umri wa miaka minane alikamatwa wakati alisafiri peke yake kutoka chini Comoro akitumia pasipoti ambayo haikuwa yake.

Wakili wa kikundi kinachowatetea watoto aliiambia BBC kuwa wanapinga kurudishwa kwake nyumbani siku ya Jumapili.

Aliongeza kuwa wanataka kubainia ni kiyume cha sheria kumzuia mtoto huyo.