Aliyekuwa mlinzi wa Gaddafi aumwa na nyoka

Image caption Saad Gaddafi

Aliyekuwa wakati mmoja mlinzi wa mwana wa Gaddafi ambaye baadaye alifanya kazi katika baa moja nchini Australia ameumwa na nyoka alipokuwa akifanya haja ndogo msituni.

Raia huyo wa Australia Gary Peters alikuwa mlinzi wa Saad Gaddafi ,mwana wa aliyekuwa rais wa Libya Muamar Gaddafi lakini kwa sasa anafanya kazi katika kilabu moja.

Raia huyo mwenye umri wa miaka 52 alikuwa akinywa vinywaji pamoja na marafikize baada ya kazi siku ya Jumatano wakati alipotoka ili kwenda haja ndogo.

Bwana Peter alikuwa amemaliza kufanya haja ndogo wakati nyoka huyo alipomng'ata kifundo cha mguu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Aliyekuwa rais wa Libya Muammar Gaddafi

Anasema aliona sumu ikimwagika kutoka kwa mguu wake na kuhofia kwamba angefariki.

''Nilimwagiwa sumu kidogo .Iwapo ningemwagiwa nyingi pengine ningekuwa katika jeneza alisema,'' Peters.