Kisa cha ebola charipotiwa Liberia

Haki miliki ya picha Reproducao BBC News
Image caption Mwanamke aaga dunia kutokana na ebola nchini Liberia

Maafisa wa afya katika hopitali moja mjini Monrovia nchini Liberia wamethibitisha kuwa mwanamke wa umri wa miaka 30 ameaga dunia kutokana na ugonjwa wa ebola ndani ya saa 24 zilizopita

Mkuu wa kikosi cha shughuli za dharura za ugonjw wa ebola nchini Liberia Tolbert Nyenswah alisema kuwa mwanamke huyo, alikufa alipofikishwa hospitalini katika mtaa mmoja wenye watu wengi wa New Kru katika mji mkuu Mo

Haki miliki ya picha AP
Image caption Zaidi ya watu 11,000 waliaga dunia kutokana na ebola magharibi mwa Afrika

Ilithibitihwa kuwa mwanamke huyo aliaga dunia kutoka na ugonja wa Ebola. Chanzo cha ugonjwa kinachunguzwa kwa kuwa ndicho kisa cha kwanza tangu Liberia itangazwe kuwa isiyo na ugonjwa wa ebola kwa mara ya tatu mwezi Januari,

Katika taifa jirani la Guinea visa kadha vya ugonjwa wa ebola vimetambulia wiki chache zilizopita. Zaidi ya watu 11000 waliaga dunia kutoka na ugonja wa ebola kwa zaidi ya miaka miwili wengi nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea.