Nigeria kurudisha pesa zilizoibiwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani John Kerry.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani John Kerry ameahidi kuisaidia Nigeria kurudisha pesa za serikali zilizoibiwa na kufichwa kwenye benki za Marekani.

Bwana Kerry alimhakikishia hilo rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, kwenye mazungumzo kati yao mjini Washington.

Taarifa zinasema kuwa maafisa wa Marekani watakutana na kitengo cha kupambana na ufisadi cha Nigeria kuzungumzia zaidi suala hilo.

Bwana Buhari amechukua msimamo mkali dhidi ya ufisadi katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta tangu aingie ofisi mwaka uliopita.