Upinzani waapa kumng'oa Zuma mamlakani

Haki miliki ya picha
Image caption (kulia) Kiongozi wa chama cha EFF Julius Malema.

Kiongozi wa mrengo wa kushoto nchini Afrika Kusini Julius Malema ameonya kuwa chama chake kitamzuia Rais Jacob Zuma kuhutubia bunge kufuatia uamuzi ulitolewa na mahakama ya juu zaidi nchini humo kuwa alikiuka katiba kwa kukataa kuilipa serikali pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba yake binafsi.

Amesema kuwa chama chake cha Economic Freedom Fighters kitashinikiza kuondolewa kwa Rais Zuma na kuvunjwa kwa bunge ili kufanyika uchaguzi wa mapema.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Makao ya Zuma yaliyofanyiwa ukarabati.

"Kati ya sasa na wakati wa kumuondoa madarakani, Rais hatuzungumza bungeni. Tutamzuia.Tutamsukuma." Malema alismema.

Upinzani uliwasilisha kesi mahakamani baada ya bwana Zuma kupuuza uamuzi wa mwaka 2014 kuwa alinufaika kutokana na ukarabati wa nyumba yake na kwamba alistahili kulipa pesa zilizotumiwa.

Mahakama ilisema kwa wizara ya fedha itatambua ni kiasi gani cha pesa kilichotumiwa na kwamba Zuma atalipa yenye mwenyewe.