Mwanasiasa wa ANC amtaka rais Zuma kujiuzulu

Haki miliki ya picha
Image caption Jacob Zuma

Mwanasiasa anayeheshimiwa wa chama tawala cha Afrika Kusini ANC , Ahmed Kathrada, amejumuika na watu wanaoengezeka, ambao wametoa wito kwa Rais Jacob Zuma ajiuzulu.

Siku ya Alhamisi, mahakama kuu ya nchi, ilisema kuwa rais amekwenda kinyume na katiba, katika kashfa ya mamilioni ya dola, yaliyotumiwa kutengeneza nyumba yake binafsi.

Bwana Kathrada, ambaye alifungwa kwa miaka mingi katika kisiwa cha Robben, pamoja na Nelson Mandela, alisema, Rais Zuma atazidisha watu kukosa imani na serikali ya Afrika Kusini, ikiwa atabaki madarakani,.

Rais Zuma amesema wazi kuwa hana azma ya kujiuzulu.