UN kutuma wanajeshi nchini Burundi

Haki miliki ya picha
Image caption Banki-moon na rais wa Burundu Pierre Nkurunziza

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio la kuweka mikakati ya kuwatuma wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi, ambapo vita vya kisiasa vilivyochukua takriban mwaka mmoja vinatishia kuwa vita vya kikabila.

Azimio hilo lililowasilishwa na Ufaransa limeutaka Umoja wa Mataifa kuweka mpango madhubuti wa kuwatuma maafisa wa kurejesha amani kwa ushirikiano na serikali ya Burundi.

Hata hivyo rais wa Burundi , Pierre Nkurunziza, amepinga hatua yoyote ya kuingilia kati Umoja wa Mataifa na pia Umoja wa Afrika.

Zaidi ya watu 400 wameuawa na robo milioni kutafuta hifadhi katika mataifa jirani tangu kuzuka kwa vurugu hizo mwaka uliopita.