Marekani: Muda unayoyoma kwa Burundi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Burundi

Afisa wa daraja ya juu wa Marekani, anasema wakati unapita kwa serikali ya Burundi.

Nchi hiyo imekuwa katika ghasia tangu mwaka jana, pale Rais Pierre Nkurunziza alipoamua kuwania muhula wa tatu wa uongozi.

Mamia ya watu wameuawa tangu wakati huo, na milioni moja wamekimbia.

Marekani na Umoja wa Ulaya zimeiwekea vikwazo Burundi.

Wakati akizuru Burundi, waziri mdogo wa Marekani anayeshughulika na haki za kibinaadamu, demokrasi na ajira, (Tom Malinowski), alisema karibu serikali itapata shida kujiendeleza na kulipa wanajeshi.