Obama: Trump haelewi sera za kigeni

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Obama

Mgombea wa kiti cha urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump, hana ufahamu wowote wa sera za kigeni wala maswala ya ulimwengu!

Haya ni kulingana na rais wa Marekani Barrack Obama.

Obama ameyasema haya kufuatia matamshi ya Donald Trump kuwa wanajeshi wa Marekani wanafaa kuondoka Japan na Korea Kusini, na mataifa hayo yanafaa kutengeneza zana zao za kinyuklia.

Image caption Trump

Mataifa hayo mawili pia hayakufurahishwa na matamshi ya bwana Trump.