Viongozi 72 duniani wahusika na kampuni ya siri

Image caption Nyaraka za siri zilizopatikana zaonesha kuwa viongozi 72 kote duniani wanatumia kampuni moja kutakatisha fedha kukwepa kodi

Stakabadhi za siri za shirika moja la kisheria la Panama zilizopatikana na gazeti moja la Ujerumani zimeonyesha viongozi zaidi ya 72 wakuu wa nchi wa zamani na wale waliopo madarakani wanahusika na kampuni hiyo ya kisiri iliyowasaidia wateja wao kukwepa kulipa kodi, utakatishaji fedha, kukiuka mikataba na vikwazo vya kiuchumi vya kimataifa.

Kwa mujibu wa nyaraka za siri zilizopatikana na gazeti moja la Kijerumani na kusomwa na Idhaa ya BBC, kampuni hiyo ya Mossack Fonseca imewasaidia watu duniani kote kufungua kampuni kwenye visiwa ambavyo havitozi kodi.

Hati hizo zinaonyesha kuwa dola bilioni kadhaa zilitakatishwa na benki moja ya Urusi kwa kumuhusisha mtu mwenye uhusiano na rais Urusi Vladimir Putin.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Viongozi 72 duniani washirikishwa na kampuni ya siri ya Panama

Nyaraka za kampuni hiyo ya Mossack Fonseca zinaonesha kampuni zote zilizofunguliwa kwenye visiwa vinavyotoa misamaha ya kodi zilifuata sheria na miiko ya ufunguaji biashara.

Mossack Fonseca imesema inasikitika kuwa kuna ambao wametumia vibaya huduma zake.