Syria: Jamii ya Alawite sasa yamtenga Assad

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jamii ya Alawite sasa yamtenga Assad

Baadhi ya viongozi kutoka kabila la Rais Bashar al-Assad la Alawite nchini Syria, wamejitenga rasmi na serikali yake.

Hayo ni kwa mjibu wa taarifa zilizopatikana na BBC.

Viongozi hao wanasema kuwa wanatarajia kutoa mwanga kwa watu wa kabila la Alawite, baada ya muda mrefu wa kukaa sirini.

Sasa wanasisitiza kuwa watu wa kabila hilo, hawafai kujihusisha na kile wanachokitaja kuwa uhalifu unaotekelezwa na utawala huo wa rais Assad.

Viongozi hao wanatoa wito wa kutotengwa katika utawala ujao wa Syria.

Image caption Viongozi hao wanatoa wito wa kutotengwa katika utawala ujao wa Syria.

Aidha wanapendekeza mfumo mpya wa serikali ya baadaye ambao Uislamu, Ukristo na madhehebu mengine yako sawa.

Watu wa kabila la Alawite, wamekuwa wakiajiriwa kwa wingi ndani ya idara ya usalama wa taifa chini ya uongozi wa Bwana Bashar al- Assad na hayati babake kwa zaidi ya miongo minne.

Ukabila na utengano, umekuwa mojawepo ya kiini kikuu katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.