Waandishi wa BBC watimuliwa Djibouti

Image caption Rais Ismail Omar Guelleh anawania hatamu ya nne uongozini.

BBC imeiandikia serikali ya Djibouti kuuliza ni kwanini kundi la waandishi wake wa habari walizuiwa kwa saa 16 na baadaye kutimuliwa nchini humo.

Waandishi hao waliopata idhini ya kufanya kazi nchini humo walikwenda huko kuripoti kuhusu uchaguzi wa urais wa Ijumaa ijayo.

Rais Ismail Omar Guelleh anawania hatamu ya nne uongozini.

Katika taarifa ya BBC, Idhaa hii ilikuwa na kibali maalum cha kutekeleza wajibu wao nchini humo.

Hadi kufikia sasa haijulikani kwanini walifurushwa kwani walikuwa wamefanya mahojiano na waziri wa maswala ya nje Mahamoud Ali Youssouf na mmoja wa viongozi wa upinzani anayegombea katika uchaguzi huo bwana Omar Elmi Khaireh.

Walikamatwa na maafisa waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia.

Image caption Waandishi wa BBC wafurushwa Djibouti

Walihojiwa kwa zaidi ya saa 8.

Wakawekwa korokoroni bila njia yeyote ya mawasiliano kabla ya kufurushwa jumamosi asubuhi bila maelezo yeyote.