Nigeria yaomba msamaha kwa ukosefu wa mafuta

Image caption Nigeria yaomba msamaha kwa ukosefu wa mafuta

Waziri wa Mafuta wa Nigeria ameomba radhi wa taifa zima baada ya ukosefu wa mafuta kusababisha maelfu ya wasafiri kukwama mabarabarani wakati wa sikukuu ya pasaka.

Waziri Emmanuel Ibe Kachikwu ameelezea ''uchungu'' uliosababishwa na upungufu huo wa mafuta ya magari.

Bw Kachikwu ameahidi kumaliza kabisa upungufu wa aina hiyo kote nchini.

Aidha amesema kuwa serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwepo kwa mafuta nchini humo.

Haki miliki ya picha none
Image caption Wenye magari wanasema kuwa wakati mwengine wanalazimika kupiga foleni kwa masaa mengi mno .

Katika majuma kadhaa yaliyopita foleni ndefu ya magari pikipiki na hata lori imeshuhudiwa kwenye vituo vya kuuzia bidhaa hiyo adimu.

Wenye magari wanasema kuwa wakati mwengine wanalazimika kupiga foleni kwa masaa mengi mno .

Wengi wanajiuliza itakuwaje kuwa Nigeria ndilo taifa linalozalisha idadi kubwa zaidi ya mafuta barani Afrika ilhali hata nyumbani hawana mafuta ya magari?

Haki miliki ya picha none
Image caption Wauzaji mafuta wanasema kuwa kuna utashi mkubwa wa dola za Marekani wanazohitaji kununua mafuta.

Wasilolijua ni kuwa Nigeria haina mtambo wa kusafisha mafuta na hivyo lazima iagize kutoka nje mafuta ya matumizi yake ya nyumbani.

Wauzaji mafuta wanasema kuwa kuna utashi mkubwa wa dola za Marekani wanazohitaji kununua mafuta.

Lakini kuna madereva wanaoshuku utashi huo wakidai kuwa huenda ni njama ya wauzaji mafuta kuongeza bei ya bidhaa hiyo