Senegal kupokea wafungwa wa Guantanamo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Senegal kuwapokea wafungwa wa Guantanamo

Senegal imekubali kuwapokea wafungwa wawili wa Guantanamo Bay kwa misingi ya kibinadamu .

Serikali ya taifa hilo la Magharibi mwa Afrika inasema kuwa kutokana na mafunzo ya dini ya kiislamu wamekubalika kuwapokea walibya hao 2 kwa mujibu wa waziri wa maswala ya kigeni wa nchi hiyo.

Wafungwa hao 2 walikuwa wanatumikia kifungo cha miaka 14 jela bila kufunguliwa mashtaka yeyote.

Kauli hiyo inafuatia uamuzi wa serikali ya rais Barack Obama ya kufunga jela hiyo ya kisiwa cha Guantanamo Bay.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafungwa hao 2 walikuwa wanatumikia kifungo cha miaka 14 jela bila kufunguliwa mashtaka yeyote.

Rais huyo wa Marekani aliahidi kufunga kituo hicho miaka 7 iliyopita.

Mataifa machache yamekubali kuwapokea wafungwa wa Guantanamo Bay yakiwemo baadhi ya mataifa ya kiafrika kama Uganda, Ghana na Cape Verde.