Ufaransa yajiandaa kwa "Euro 2016"

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bernard Cazeneuve

Wafanyakazi wa huduma ya dharura nchini Ufaransa wamefanya zoezi la kujihami na mashambulizi ya kigaidi katika viwanja vya mpira na maeneo mengine yatakayotumika kwa mashindano ya mpira barani ulaya yanayotarajiwa kuanza mwezi June.

Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo, Bernard Cazeneuve amesema serikali yake imeamua kufanya jaribio hilo ili kuhakiki kuwa mfumo mzima utawezesha michuano hiyo ya "Euro 2016" kwenda salama kutokana na tishio la usalama dhidi ya nchi hiyo .

Wakati waziri wa afya , Marisol Touraine amesema maandalizi hayo yamefanyika kama tahadhari ili tukio la Novemba mjini Paris lisijirudie.