Aung Suu Kyi kuwa waziri mkuu Myanmar

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Aung Suu Kyi

Bunge la Myanmar limepitisha mswada wa kuunda nafasi kuu rasmi ya kiongozi anayeunga mkono demokrasia, Aung San Suu Kyi.

Wadhifa huo ni sawa na ule wa waziri mkuu wa nchi.

Mwandishi wa BBC anasema wabunge ambao hawakuchaguliwa kutoka jeshi lililokuwa likiitawala nchi, wamesusia kura hiyo na kusimama katika kulalamika wakati mswada huo ulipoidhinishwa.

Sheria hiyo sasa inahitaji kuidhinishwa na rais Htin Kyaw, ambaye ni mshirika wa karibu wa Aung San Suu Kyi.