Makamanda sita wa al-Shabab wauawa Somalia

Amisom Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Amisom wamekuwa wakikabiliana na wapiganaji wa al-Shabab

Kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika nchini Somalia kimesema makamanda sita wa kundi la wapiganaji wa Kiislamu la al-Shabab wameuawa na wanajeshi hao wakishirikiana na wanajeshi wa Somalia.

Wapiganaji hao wameuawa eneo la Janaale.

Kikosi hicho kimesema, kupitia taarifa, kwamba kamanda mwingine Abdirashir Bugdube aliyeuawa wiki iliyopita.

Amisom wamesema miongoni mwa sita hao kulikuwa na raia wa Yemen ambaye alikuwa mtaalamu wa kuunda mabomu na raia wa Kenya ambaye alikuwa mkufunzi mkuu.

Al-Shabab bado hawajazungumzia taarifa hiyo ya Amisom.