Faini ya dola laki 6 kwa kumiliki pembe ya ndovu

Image caption Faini ya dola laki 6 kwa kumiliki pembe ya ndovu

Wanaume wawili waliopatikana na hatia ya uwindaji haramu wamepigwa faini ya dola laki 630,000 na mahakama nchini Kenya.

Katika kisa cha kwanza Wilson Kiyayooni alipatikana na hatia ya kulabgua kilo 3 ya pembe ya ndovu.

Hakimu wa mji wa mji wa Narok Kusini mwa Kenya Allan Sitati, alimhukumu kifungo cha maisha jela la sivyo alipe faini ya dola laki nne ($400,000)

Na katika kisa cha pili, Laikipia, eneo la kati ,James Aoi Lokigen alifikishwa mbele ya hakimu mwandamizi wa Nyahururu Peter Ndege, aliyemhukumu kifungo cha maisha jela kwa kumiliki kilo tatu za pembe kinyume cha sheria.

Lokigen alipigwa faini ya dola laki mbili, (230,000)

Mahakama nchini Kenya zimeimarisha faini zinazotoza washukiwa wa biashara haramu ya uwindaji wanyama pori.