Nyaraka za panama zawazonga wanasiasa Nigeria

Bukola Saraki Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Seneti Bukola Saraki anakaba kuhusika na kosa lolote la umiliki wa mali isiyo halali

Shinikizo kubwa zinaendelea kuwazonga viongozi wakuu zaidi wa kisiasa nchini Nigeria kuachia madaraka kufuatia tuhuma zilizotolewa na magazeti yaliyofichua data kuhusu ukwepaji wa kodi.

Rais wa Seneti Bukola Saraki - kwa sasa anashtakiwa mahakamani kwa tuhuma za kununua mali kwa pesa zilizoibiwa na kushindwa kutangaza mali zake.

Katika tukio jingine taarifa kutoka kwenye magazeti ya Panama zilisema kuwa wanasiasa hawakutangaza mali zao zisizo halali zilizoorodheshwa chini ya jina la mkewe.

Bwana Saraki anakana kufanya kosa lolote lile.

Kutangazwa kwa taarifa za magazeti ya Panama kumekuja wakati ambapo taarifa zimejitokeza kuhusu shutuma mpya zinazomuhusisha bwana Saraki na masuala ya kifedha.

Haki miliki ya picha State House
Image caption Alipoingia mamlakani rais Buhari aliahidi kuung'oa ufisadi Nigeria

Magazeti ya Nigeria - Premium Times -moja ya magazeti yanayofanyia kazi magazeti ya Panama Papers, limeripoti kwamba familia ya mwanasiasa huyo inamiliki mali za aina nne ambazo haijatangaza , zikiwemo mali zenye thamani ya mamilioni ya dola mjini London .

Saraki amekana mashtaka kumi na tatu dhidi yake kuhusiana na miaka makosa aliyoyafanya alipokua gavana wa jimbo.

Tangu alipochaguliwa mwaka jana rais wa Nigeria Muhammadu Buhari aliahidi kung'oa ufisadi serikalini .Ikiwa atapatikana na hayia, Bwana Saraki anaweza kuzuiwa kuongoza ofisi ya umma na kukabiliwa na kifungo cha jela.