Huwezi kusikiliza tena

Kampuni ya mafuta ilitaka kukwepa kodi Uganda

Ushahidi mpya uliotokana na nyaraka zilizofichuliwa za Panama zimefichua jinisi kampuni ya kuchimba mafuta iliyopo Uingereza iliyo na uhusiano na chama tawala ilivyojaribu kukwepa kulipa dola milioni 400 za kodi kwa serikali ya Uganda.

Barua pepe zilizofichuliwa na muungano wa waandishi wapelelezi wa kimataifa ICIJ na zilizosambazwa kwa BBC zinaonyesha kuwa kampuni hiyo ilifahamu kuhusu malipo hayo ya kodi yanayohusu uuzaji wa hisa zake katika biashara ya mafuta Uganda.

Mapendekezo yaliwasilishwa baadaye ili kukwepa kulipa deni hilo kwa kuhamisha usajili wa kampuni hiyo kutoka Bahamas hadi Mauritius.