Boko Haram 800 wajisalimisha Nigeria

Haki miliki ya picha BOKO HARAM VIDEO
Image caption Wapiganaji 800 wa kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram wamejisalimisha kwa Jeshi la Nigeria.

Wapiganaji 800 wa kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram wamejisalimisha kwa jeshi la Nigeria.

Hatua hiyo inafuatia mpango mahsusi wa 'Operation Safe Corridor' unaolenga kuwapokea wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi ambalo limesababisha vifo vya maelfu ya raia wa Nigeria.

Chini ya mpango huo wapiganaji wanaojisalimisha wanachukuliwa na kufunzwa upya njia mbadala ya kujitafutia riziki.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Msemaji wa jeshi amesema kuwa wanania ya kuwasamehe wapiganaji wa Boko Haram watakaotubu makosa yao.

Msemaji wa jeshi amesema kuwa wanania ya kuwasamehe wapiganaji wa Boko Haram watakaotubu makosa yao.

Kwa sasa wamewekwa kwenye makazi maalum ambapo wanaendelea kupata mafunzo ya msimamo wastani wa kidini.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakaazi milioni moja wanaishi katika kambi za wakimbizi wa ndani kwa ndani

Baadaye watafunzwa mbinu mpya za kujitafutia riziki kabla ya kupewa mtaji wa kuanza upya maisha yao.

Hata hivyo kuna hofu iwapo jamii itakuwa tayari kuwapokea wapiganaji waliotekeleza maasi dhidi yao.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Zaidi ya watu 10,000 waliuawa huku takriban wakaazi milioni moja wakitoroka makwao tangu uasi huo uanze yapata miaka 7 iliyopita.

Wahanga wa maasi yao ndio wanaotarajiwa kuwa na wakati mgumu zaidi kuwapokea ama hata kuwasamehe wapiganaji hao wa zamani.

Eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria ndilo lililoathirika sana na mashambulizi ya Boko Haram.

Zaidi ya watu 10,000 waliuawa huku takriban wakaazi milioni moja wakitoroka makwao tangu uasi huo uanze yapata miaka 7 iliyopita.