Putin akana madai ya utakatishaji fedha

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Urusi Vladimir Putin

Rais wa Urusi Vladimir Putin amekanusha madai ya kutakatisha mabilioni ya pesa.

Rais Putin anasema kuwa hakuna ukweli wowowte katika madai hayo na kuwa hizo ni njama za mahasidi wake za kutaka kuiyumbisha serikali yake.

Putin alikuwa akizungumzia kwa mara ya kwanza kasha la nyaraka za siri za kampuni moja ya kisheria ya Panama, Mossack Fonseca iliyomtaja mshirika wake mmoja wa karibu kuwa alitakatisha mabilioni ya dola .

Stakabadhi hizo za siri za Mossack Fonseca zilizopatikana na gazeti moja la Ujerumani zilionyesha kuwa viongozi zaidi ya 72 wakuu wa nchi wa zamani na wale waliopo madarakani wanahusika na kampuni hiyo ya kisiri iliyowasaidia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mossack Fonseca zilizopatikana na gazeti moja la Ujerumani

Wateja wake kukwepa kulipa kodi, utakatishaji fedha, kukiuka mikataba na vikwazo vya kiuchumi vya kimataifa.

Aidha kampuni hiyo ya Mossack Fonseca imewasaidia watu duniani kote kufungua kampuni hewa kwenye visiwa ambavyo havitozi kodi.

Hati hizo zinaonyesha kuwa dola bilioni kadhaa zilitakatishwa na benki moja ya Urusi kwa kumuhusisha mtu mwenye uhusiano wa karibu na rais Urusi Vladimir Putin.