Mji wa Al-Rai-Syria wakombolewa

Haki miliki ya picha Reuters

vikosi vya waasi wa Syria wamevirejesha nyuma vikosi vya wanamgambo wa dola ya kiislamu wa Islamic State nje ya mji ambao pande zote mbili wanauwinda kuwa chini ya himaya yake upande wa Kaskazini mwa Syria, baada ya siku kadhaa za mapambano makali.

Mji wa Al-Rai,ulioko jirani na jimbo la Aleppo ,ni ngome ya wanamgambo hao wa IS ambao uko kwenye mpaka unaoingia nchini Uturuki hadi kuingia Syria.

Waasi hao wa Syria wamewahi kuhusika na matukio ya kukera ingawa hupigana chini ya jeshi huru la Syria ambalo limekuwa likiwagawia silaha kutoka nchin Uturuki.