Mvulana aokolewa baada ya kutuma ujumbe 'Sipati hewa'

Image caption Mvulana aliyesafishwa ndani ya kasha hadi nchini Uingereza kutoka Calais

Mvulana mmoja raia wa Afghanistan ambaye alikuwa ndani ya lori aliokolewa na maafisa wa polisi wa Uingereza baada ya kutuma ujumbe kwamba anakosa hewa.

Mvulana huyo ,ambaye alikuwa akitumia simu aliopewa na shirika moja la wahisani huko Calais,alisema kuwa anakabiliwa na upungufu wa ''Oksijan'' akimaanisha Oxygen {hewa}.

Yeye na watu wengine 14 walipatikana katika kasha baada ya kuwasii kutoka kambi ya wakimbizi ya Calais inayojulikana kama The Jungle.

Maafisa wa Polisi wa Leicestershire wamesema kuwa kundi hilo la wahamiaji lilipatikana ndani ya kasha la lori la huduma za misitu mashariki mwa Leicester.

Maafisa hao wamesema kuwa maafisa wa uhamiaji wameichukua kesi hiyo na kuweka mikakati ya kumlinda mvulana huyo.

Hakuna mtu aliyepelekwa hospitalini.