Shindano la American Idol lafikia kikomo

Image caption Amerian Idol

American Idol imekamilika.Kipindi hicho kimekamilika huku mtangazaji wake Ryan Seacrest akikikamilisha kwa mara ya mwisho.

Tangu mwaka 2002 kipindi hicho kilisaidia kuzindua ajira kwa wasanii wengi akiwemo Kelly Clarkson na Jennifer Hudson.

Ni kipindi kilichopendwa sana katika runinga za Marekani kwa miaka saba mfululizo,huku fainali za kipindi cha mwaka 2003 zikipata watazamaji wengi zaidi ya tuzo za Oscar.

Tamasha la Idol lilianza mwaka 2001 nchini Uingereza,na kumsaidia mfanyibiashara mmoja wa muziki ambaye hakuwa akijulikana Simon Cowel kutawala ulimwengu wa muziki.

Wakati huo wazo la kuwasaidia wale wenye vipawa vya kuimba mitaani kuwa nyota halikuwepo.Lakini mafanikio yake nchini Uingereza yalikuwa kiwiliwili kilipoanzishwa nchini Marekani na kuimarika.

Image caption Majaji wa Amarican Idol

Waanzilishi wake walikifanya kipindi hicho kuwa cha msururu wa msimu ,lakini kufikia fainali za msimu wa pili takriban watazamaji milioni 38 walianza kukitazama.

Kwa miaka kadhaa idadi hiyo imepungua ijapokuwa wengi wanasema kuwa kilianguka na kufikia viwango vya kawaida na wala sio vya kupita kiasi.

Hatahivyo mwanzilishi wa Tamasha hiyo Simon Fuller alisema kuwa Idol huenda ikarudi siku zijazo.

''Bila shaka kutakuwa na mpango mpya uliopigwa msasa wa kipindi hicho.Sasa naweza kukiimarisha na kuleta toleo jipya'', aliongezea.