Mshukiwa muhimu wa shambulio la Paris akamatwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mohamed Abrini

Mshukiwa muhimu wa shambulio la kigaidi la mwezi Novemba mjini Paris ,Mohamed Abrini amekamatwa,vyombo vya habari vya Ubelgiji vimesema.

Duru za vyombo hivyo vya habari zinasema kuwa Abrini ni mtu anayeshukiwa kuvaa kofia aliyeonekana katika kanda ya CCTV kabla ya mlipuko katika uwanja wa ndege wa Brussels mnamo tarehe 22 mwezi Machi.

Waendesha mashtaka wamethibitsha kwamba watu kadhaa walikamatwa kuhusiana na shambulio hilo la Brussels.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Picha ya Mohamed Abrini

Shambulio hilo la Paris mnamo mwezi Novemba liliwaua watu 130.

Vyombo vya habari vinasema kuwa Abrini ambaye amekuwa mafichoni kwa takriban miezi mitano alikamatwa wilayani Anderlecht huko Brussels.