Ruto: Waathiriwa wa ghasia lazima wapate haki

Haki miliki ya picha DPPS Kenya
Image caption William Ruto

Naibu wa rais nchini Kenya William Ruto amevihutubia vyombo vya habari kwa mara ya kwanza tangu kesi iliokuwa ikimkabili kuhusiana na ghasia zilizotokea katika uchaguzi wa mwaka 2007 katika mahakama ya ICC ifutiliwe mbali.

Ruto amesema kwamba serikali haitapumzika hadi waathiriwa wa gjhasia hizo ambapo takriban watu 1200 walifariki wapate haki yao.

''Sababu ambayo iliofanya kesi hiyo kuanguka ni kwamba hatukuwa na hatia''.