Ndovu afanya uharibifu kwa mara ya pili China

Haki miliki ya picha APTN
Image caption Ndovu afanya uharibfu nchini China

Ndovu mmoja amesababisha hasara kubwa na majeruhi nchini Uchina kwa mara ya pili katika kipindi cha miezi michache iliyopita.

Ndovu huyo kwa jina Zhusunya, aliwashambulia wafanyakazi watoto ambao walikuwa wakirekebisha nyaya katika hifadhi moja ya wanyama katika mkoa wa kusini wa Yunnan.

Mmoja wa wafanyakazi hao alijeruhiwa huku wawili wakifanikiwa kutoroka.

Februari mwaka huu, ndovu huyo aliharibu magari kadhaa yaliyokuwa yameegeshwa kando ya barabara katika hifadhi hiyo.

Eneo hilo ndilo makaazi ya ndovu wa mwituni waliosalia nchini Uchina, ambako inakadiriwa kuwa mia tatu pekee ndio waliosalia.