Kundi la Abu Sayyaf lamwachilia kasisi Mtaliano

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watekaji wa kundi la Abu Sayyaf

Aliyekuwa kasisi wa Italia ambaye alizuiliwa mateka nchini Ufilipino kwa miezi sita, ameondoka hospitalini baada ya kuachiliwa huru.

Rolando Del Torchio alitekwa nyara na wapiganaji wa kundi la Kiislamu la Abu Sayyaf, Oktoba mwaka uliopita.

Msemaji wa jeshi nchini humo amesema haijulikana ikiwa wanamgambo hao walilipwa kikombozi ili kumuachilia huru.

Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa kundi hilo lililipwa zaidi ya dola laki sita .

Kundi la Abu Sayyaf limefahamika kwa vitendo vyake vya kuwateka nyara raia wa kigeni na kuitisha kiasi kikubwa cha pesa ili kuwaachilia huru.