Uchaguzi wa urais wafanyika Chad

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Deby ameongoza nchi hiyo kwa miaka 26

Upigaji kura umekamilika nchini Chad, katika uchaguzi wa urais, ambapo Rais Idriss Deby anatarajiwa kushinda muhula wake wa tano.

Rais Deby ameongoza nchi hiyo kwa miaka 26, tangu aliponyakua madaraka katika mapinduzi.

Maandamano ya kumtaka aondoke madarakani yamepigwa marufuku, na wanaharakati wamefungwa.

Mshindani mkuu wa Rais Deby, Saleh Kebzabo, anasema, rais huyo amejaribu kuwanyamazisha, katika kampeni ya uchaguzi.

"serikali imeazimia kukandamiza demokrasia, na haiheshimu kanuni za msingi, za kura ya siri ---wanafanya kusudi kuzuwia wananchi kuchagua watakaye.

Lakini juu ya yote hayo, dhamira ya watu wa Chad haiyumbi.

Image caption Kiongozi wa upinzani Saleh Kebzabo

Na utatambua hayo mwisho wa kura."alisema Saleh Kebzabo

Rais Deby alikanusha madai ya wapinzani wake akisisitiza kuwa uchaguzi huu utakuwa wa huru na wa haki.

'' Nataka kuwahakikishia raia wa Chad kuwa uchaguzi huu utakuwa huru na wa haki.''

''Ningependa kuwasihi kutoka moyoni mwangu mjitokeze kwa wingi mchague yule mnayemtaka awaongoze ''.

''Hakuna shinikizo lolote.''

Haki miliki ya picha
Image caption Mshindani mkuu wa Rais Deby, Saleh Kebzabo, anasema, rais huyo amejaribu kuwanyamazisha, katika kampeni ya uchaguzi.

''Kila kitu sharti liwekwe sawa ''.

''Chad inapaswa kuibuka yenye umoja baada ya uchaguzi huu'' .

''Licha ya kukabiliwa na changamoto nyingi sharti tuelewe sisi wenyewe ,hata mimi nimeelewa'' alisema rais Idriss Deby

Licha ya kuibuka kuwa moja ya mataifa yanayozalisha mafuta barani Afrika, nusu ya watu wa Chad yaani takriban watu milioni tano hivi wanaishi katika umaskini mkubwa.