Marekani yakosoa kura ya maoni Darfur

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Marekani yakosoa kura ya maoni Darfur

Marekani imesema ina wasiwasi kuhusu kura ya maoni itayofanywa Darfur na serikali ya Sudan hapo kesho.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka katika eneo hilo magharibi mwa Sudan, mwaka 2003, na vingali vinaendelea.

Image caption Marekani inasema kwa vile hakuna usalama, na baadhi ya watu wamekimbia makwao kwa sababu ya vita

Katika kura hiyo ya maoni, wananchi wataamua ikiwa wanataka Darfur iwe jimbo moja kwa kuunganisha majimbo matano ya hivi sasa, au la.

Wapiganaji wa Darfur kwa muda mrefu wamedai kuwa Darfur iwe jimbo moja, huku serikali ikitaka ibaki na majimbo matano kurahisisha utawala.

Marekani inasema kwa vile hakuna usalama, na baadhi ya watu wamekimbia makwao kwa sababu ya vita, kura hiyo ya maoni haiwezi kuendeshwa sawasawa.

Image caption Marekani inapendekeza wangesajiliwa wenyeji wote wa Darfur kabla ya kufanyika kura hiyo ya maoni.

Aidha Serikali inahoji usawa wa kura hiyo ya maoni utafanyikaje ilhali raia wengi wenyeji wa Darfur wametoroka makwao wanaishi katika kambi za wakimbizi wa ndani kwa ndani ?

Marekani inapendekeza wangesajiliwa wenyeji wote wa Darfur kabla ya kufanyika kura hiyo ya maoni.