Tetemeko la ardhi latikisa Asia Kusini

Haki miliki ya picha AP
Image caption Tetemeko hilo lilitikisa majengo nchini Pakistan, Afghanistan, na kaskazini mwa India.

Tetemeko kubwa la ardhi, la kipimo cha 6.6 kwenye vipimo vya Richter limetikisa maeneo ya Kusini-Magharibi mwa Asia.

Kitengo cha ardhi cha Marekani, kinasema kitovu cha tetemeko kiko karibu na eneo la milima, katika mpaka baina ya Afghanistan na Pakistan, kilomita 200 chini ya ardhi.

Tetemeko hilo lilitikisa majengo nchini Pakistan, Afghanistan, na kaskazini mwa India.

Mijini Islamabad na Kabul, watu walishtuka na kukimbia nje, kutoka majumbani mwao na maofisini, wakati majengo yalianza kuyumbayumba.

Image caption Kitovu cha tetemeko hilo la ardhi ilikuwa karibu na mapaka wa Afghanistan na Pakistan

Tetemeko lilisikika piya katika mji mkuu wa India, Delhi na maeneo yanayozunguka.

Treni za mji mkuu wa New Delhi zilisimamishwa kwa muda.

Bado hakuna taarifa ya maafa yoyote.