Utafiti: Plastiki yapatikana ndani ya Samaki

Image caption Utafiti: Plastiki yapatikana ndani ya Samaki

Je unapenda kula samaki ?

Ikiwa unapenda Dagaa Pweza,Pelege,Mwatiko, Papa, Kiduwa, Kambale,Tilapia ama samaki wa aiana yeyote yule basi unapaswa kusoma taarifa hii ya utafiti.

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Watafiti kutoka chuo cha Kilimo na Teknolojia cha Tokyo, wamekuta chembe chembe za plastiki katika asili mia 80% ya matumbo ya dagaa

Wanasayansi nchini Japan wanasema wamekuta plastiki nyingi ndani ya mwili wa samaki, katika bahari inayozunguka Japan.

Watafiti kutoka chuo cha Kilimo na Teknolojia cha Tokyo, wamekuta chembe chembe za plastiki katika asili mia 80% ya matumbo ya dagaa, waitwao 'anchovies'', waliovuliwa katika bahari iliyoko nje ya Tokyo.

Image caption Chembechembe ambazo zinaingia ndani ya matumbo ya samaki na ndege.

Chembechembe za plastiki, kutokana na mifuko ya plastiki au urembo, zinanyonya kemikali za sumu, ambazo zinaingia ndani ya matumbo ya samaki na ndege.

Plastiki hizo zimepatikana katika samaki wa Marekani, Uingereza, hadi Indonesia, pia katika nyangumi, chaza na ndege wa pwani.