Buhari afanya ziara China

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Muhammadu Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anafanya ziara nchini China ambapo anatarajiwa kutia sahihi mikataba kadha ya kibiashara na uwekezaji baadaye wiki hii.

Pia bwana Buhari anatarajiwa kufanya mazungumzo na rais wa China Xi Jinping.

Tangu achukue hatamu za uongozi mwaka uliopita, kiongozi huyo wa Nigeria amekuwa akifanya ziara kujaribu kuinua uchumi wa nchi hiyo ambao umeathirika kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uchumi wa Nigeria umeathirika kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani.

Wajibu wa rais Buhari nchini China ni kupata mikopo ya kuziba pengo la dola milioni 10 katika bajeti yake.

Anataka kutumia pesa hizo kuboresha miundo msingi ya nchi hiyo iliyochakaa na kuwekeza kwenye kilimo.