Misri: Waziri afungwa miaka 10 kwa ufisadi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliyekuwa Waziri wa kilimo bwana Salah Helal na msaidizi wake watatumikia miaka 10 gerezani kwa kupanga njama ya kuuza kipande cha ardhi cha umma

Mahakama moja nchini Misri imemhukumu waziri wa zamani wa kilimo miaka 10 gerezani kwa kushiriki ufisadi.

Aliyekuwa Waziri wa kilimo bwana Salah Helal na msaidizi wake watatumikia miaka 10 gerezani kwa kupanga njama ya kuuza kipande cha ardhi cha umma kwa mfanyibiashara mmoja kwa bei ya chini mno.

Aidha wawili hao walipigwa faini kubwa kufuatia upande wa mashtaka kupata ushahidi wa mfanyibiashara husika.

Waziri huyo wa zamani alikamatwa muda mchache tu baada ya kujiuzulu mnamo mwezi Septemba mwaka uliopita.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waziri huyo wa zamani alikamatwa muda mchache tu baada ya kujiuzulu mnamo mwezi Septemba mwaka uliopita.

Kashfa hiyo ilisababisha kuporomoka kwa serikali ya waziri mkuu bwana Ibrahim MahlfBoth.

Mfanyibiashara huyo na mpatanishi wake walisamehewa kifungo baada ya kukubaliana na mahakama kutoa ushahidi dhidi ya waziri.