Mawasiliano ya mitandao yakatwa Chad

Haki miliki ya picha
Image caption Mawasiliano ya simu yamekatwa tangu siku ya Jumapili

Mawasiliano kwa njia ya mitandao yamekatwa kwenye mji mkuu wa Chad siku moja baada ya rais Idriss Deby kuwania urais kuongeza ungozi wake wa miaka 26, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Mawasiliano ya intaneti kwa njia ya simu yalikatwa kuanzia siku ya Jumapili asubuhi huku ikiwa vigumu kutuma ujumbe kupitia kwa simu za mkononi.

Kukatwa huku kwa mawasiliano kulikofanyika bila kutolewa sababu, kulilenga kuzuia mawasiliano kuhusu uchaguzi huo. Wagombea 12 walishiriki kumpinga rais Deby ambaye aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi mwaka 1990.