Fifa yaitimua Equatorial Guinea

Haki miliki ya picha AP
Image caption FIFA pia imelipiga faini ya dola 40,000 shirika la kandanda la Equatorial Guinea

Timu ya kandanda ya akina dada ya Equatorial Guinea imetimuliwa na shirikisho la kandanda duniani FIFA kutoka kwa mechi za kufuzu kwa mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2020, baada ya mchezaji wake mmoja kuwasilisha tarehe tofauti za kuzaliwa.

Camila Maria do Carmo Nobre de Oliveira alitumia paspoti mbili zenye tarehe tofauti za kuzaliwa na vyeti viwili vya kuzaliwa vinavyoonyesha tofauti za wazazi kwa mujibu wa FIFA.

Shirika la Kandanda la Equatorial Guinea limepigwa faini ya dola 40,000. Huku De Oliveira akipigwa faini ya pauni 1,475 na marufuku ya mechi kumi.