Louis van Gaal aisifia Manchester

Haki miliki ya picha PA
Image caption Louis van Gaal

Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal amesema hajuti kuangushwa na Tottenham katika msimu huu wa majira wa 2014, akisema Manchester United ni 'klabu kubwa'.

Manchester United wako alama 12 chini ya Spurs baada ya kuchapwa mabao 3-0 katika uwanja wa White Hart Lane siku ya Jumamosi.

'Changamoto zilikuwa kubwa kwangu katika Manchester United na zitazidi kuwa kubwa' alisema Van Gaal , wako nafasi ya tano. ''Naomba radhi kwa Tottenham lakini Manchetser United ni Klabu kubwa''

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mancheter United ilichapwa mabao 3-0 katika uwanja wa White Hart Lane siku ya Jumamosi

Ingawaje United wamepata shida nyingi msimu huu ,Van Gaal , ambaye amekuwa akifanya mazungumzo na Spurs kuhusiana na kuwa meneja, anaamini United bado wako mbele kwa klabu za Uingereza.

Hata hivyo alimpuuzilia mbali mwanahabari ambaye alimuuliza iwapo anajutia kuchagua United dhidi ya Spurs.

'Ni jambo la kuudhi kuuliza hivyo,'' meneja huyo mwenye umri wa miaka 64 alisema. Ni rahisi kuuliza, lakini sawa wewe jifurahishe.

Baada ya Van Gaal kutia sahihi mkataba wa miaka mitatu huko Old Trafford, Tottenham imemteuwa meneja wa zamani wa Southampton Mauricio Pochettino.